Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (as) –ABNA– vita dhidi ya Gaza kila siku vinaibua sura mpya. Baada ya kushindwa kufanikisha malengo yake ya kijeshi, hususan kushindwa kuimaliza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) na kushindwa kuwaokoa mateka wa Kizayuni walioko Gaza, jambo ambalo limezua hasira za familia zao dhidi ya Netanyahu na baraza lake, sasa utawala wa Kizayuni umeweka mezani mpango wa kuikalia kwa mabavu Gaza.
“Donald Trump,” Rais wa Marekani, naye kwa upande wake, katika kitendo cha kinafiki cha kuonyesha kujali hali ya kibinadamu Gaza, ametangaza wazi kuwa Israel inayo ruhusa ya kufanya lolote dhidi ya Gaza. Hii ni pamoja na kuendeleza uungaji mkono wake wa moja kwa moja kwa jinai za Israel, hususan mabomu dhidi ya wananchi wa Palestina, na hata kushiriki moja kwa moja katika shambulizi dhidi ya mitambo ya nyuklia ya Iran. Wakati huohuo, yeye na washirika wake wanajitahidi kumtangaza kama mgombea wa Tuzo ya Amani ya Nobel.
Aidha, maigizo yake ya hivi karibuni kuhusu kuleta amani kati ya Urusi na Ukraine yameongeza mjadala huu. Hata hivyo, wachambuzi wengi wameyaona hayo kuwa ni mbinu za kisiasa za kujitangaza, zikikosa matokeo ya kivitendo katika kufanikisha makubaliano ya amani.
Katika muktadha huo, Profesa Robert Shapiro, Naibu Mkuu wa Shule ya Masuala ya Kimataifa na Umma na Profesa wa Idara ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Columbia, Marekani, amezungumza na ABNA kuhusu jinai za Israel, uungaji mkono wa Marekani, na athari za kimataifa.
ABNA: Hivi karibuni tumeshuhudia jinai kubwa Gaza: watoto wakikufa kwa njaa, waandishi wa habari kushambuliwa, na mengineyo. Wahalifu hawa wanapaswa kuchukuliwa hatua gani kisheria? Na je, jinai hizi zinaendana na madai ya Trump kuhusu msaada wa kibinadamu Gaza?
Prof. Shapiro: Kwa mtazamo wa Trump, inaonekana hana umuhimu kwa jambo hili. Anaunga mkono kufunguliwa mashtaka dhidi ya viongozi wa Hamas – yeyote aliye hai – lakini si dhidi ya viongozi wa Israel. Anailinda Israel kikamilifu. Ingawa anaweza kutaja suala la njaa Gaza, kwake si jambo la maana kiasi cha kutaka viongozi wa Kizayuni wawajibishwe.
ABNA: Hivi karibuni nchi za Ulaya na Canada zimetamka mara kwa mara kuhusu kulitambua taifa la Palestina. Je, ni msimamo wa kweli au ni mbinu ya kushinikiza Marekani?
Prof. Shapiro: Ndiyo, hili ni sehemu ya shinikizo kwa Marekani na Israel ili kusitisha vita Gaza. Lakini pia linaweza kuwa ni msimamo wa dhati. Tatizo ni kwamba serikali ya Israel na raia wengi wa Kizayuni wanaupinga vikali. Wao wanaona kuanzishwa kwa taifa la Palestina kutalazimisha Wapalestina na Waarabu kutoa mbadala wa Hamas katika kuongoza Palestina na kulisaidia.
ABNA: Vipi kuhusu shambulizi dhidi ya mitambo ya nyuklia ya Iran, licha ya kuwa mwanachama wa mkataba wa NPT (kupiga marufuku silaha za nyuklia)?
Prof. Shapiro: Hii ilikuwa siasa ya kimaada zaidi kuliko ya kimaadili. Israel ilianza vita dhidi ya Hamas na Hizbullah kwa lengo la kuziondoa ili iwe rahisi kuishambulia Iran. Baada ya anga ya ulinzi ya Iran kushambuliwa, Israel iliweza kushiriki katika mashambulizi ya nyuklia, na Trump alikubali kwa kuwa aliona fursa ya kuishambulia Iran. Mkataba wa NPT haukuwapa wasiwasi wowote. Funzo linalotokana na hili ni kuwa kama nchi inadhani inahitaji silaha za nyuklia, inapaswa kujizatiti haraka kuzipata.
ABNA: Je, unakubaliana na mapendekezo ya kumpa Trump Tuzo ya Amani ya Nobel?
Prof. Shapiro: Kitendo cha Trump kushambulia Iran kinatosha kabisa kumfanya asikubalike kupokea tuzo yoyote ya amani.
Your Comment